Huddah Monroe Sidhani Kama Nitakuja Kuolewa. ....soma hapa==>>
Huddah Monroe Sidhani Kama Nitakuja Kuolewa.
Ripota
wako wa nguvu Millard Ayo alikutana na staa mwingine wa Afrika
Mashariki wiki hii ambaye ni Huddah Monroe, Mkenya aliyewahi
kuiwakilisha nchi yake kwenye mashindano ya Big Brother Africa.Alipoulizwa
na Millard kuhusu kuolewa, Huddah alisema hadhani kama itakuja kutokea
ameolewa na sababu kuu ni anayoyaona kwa marafiki zake.
Huddah
ambaye ni mcheshi, alisema kikubwa kinachomfanya asiolewe ni yale
mateso anayoyaona kwa marafiki zake walioolewa, wanaoteswa na waume zao
huku ndoa zaobado ni changa.
Yote
haya aliyasema pamoja na kutaja sababu zilizomfanya ashindwe kuhudhuria
Zari All White Party pamoja na kwamba alikuja Dar es Salaam kwa ajili
hiyo weekend iliyopita.
Amesema
kilichomfanya ashindwe kuhudhuria ni kujisikia vibaya kiafya na wala
hakuna tatizo lolote lililotokea, anasema 'nawaheshimu na wao
wananiheshimu hivyo kusingetokea chochote kibaya, sisi ni marafiki
wazuri'.
No comments:
Post a Comment